Genesis 35

Yakobo Arudi Betheli

1 aKisha Mungu akamwambia Yakobo, “Panda uende Betheli ukakae huko na ukamjengee Mungu madhabahu huko, Yeye aliyekutokea ulipokuwa unamkimbia Esau ndugu yako.”

2 bHivyo Yakobo akawaambia watu wa nyumbani mwake pamoja na wote waliokuwa naye, “Iondoeni miungu ya kigeni ile iliyoko katikati yenu, jitakaseni na mkabadilishe nguo zenu. 3 cKisha njooni, twende Betheli, mahali nitakapomjengea Mungu madhabahu, aliyenijibu katika siku ya shida yangu, ambaye amekuwa pamoja nami popote nilipokwenda.” 4 dKwa hiyo wakampa Yakobo miungu yote ya kigeni waliyokuwa nayo, pamoja na pete zilizokuwa masikioni mwao. Yakobo akavizika chini ya mti wa mwaloni huko Shekemu. 5 eKisha wakaondoka, na hofu ya Mungu ikawapata miji yote iliyowazunguka. Kwa hiyo hakuna aliyewafuatia wana wa Yakobo.

6 fYakobo na watu wote waliokuwa pamoja naye wakafika Luzu (ndio Betheli), katika nchi ya Kanaani. 7 gHuko akajenga madhabahu na akapaita mahali pale El-Betheli,
El-Betheli maana yake Mungu wa Betheli.
kwa sababu mahali pale ndipo Mungu alipojifunua kwake alipokuwa akimkimbia ndugu yake.

8 iWakati huu Debora, mlezi wa Rebeka, akafa na akazikwa chini ya mti wa mwaloni ulioko chini ya Betheli. Kwa hiyo pakaitwa Alon-Bakuthi.
Alon-Bakuthi maana yake Mwaloni wa Kilio.


9 kBaada ya Yakobo kurudi kutoka Padan-Aramu, Mungu alimtokea tena na kumbariki. 10 lMungu akamwambia, “Jina lako ni Yakobo, lakini hutaitwa tena Yakobo, jina lako utakuwa Israeli.” Kwa hiyo akamwita Israeli.

11 mMungu akamwambia, “Mimi ndimi Mungu Mwenyezi,
Mungu Mwenyezi hapa ni jina la Kiebrania, El-Shaddai (yaani Mungu Mwenye utoshelevu wote).
ukazae na kuongezeka. Taifa na jamii ya mataifa itatoka kwako, nao wafalme watatoka viunoni mwako.
12 oNchi niliyowapa Abrahamu na Isaki nakupa wewe pia, nami nitawapa wazao wako baada yako.” 13 pKisha Mungu akapanda juu kutoka kwake mahali pale alipozungumza naye.

14 qYakobo akasimamisha nguzo ya jiwe mahali pale Mungu alipozungumza naye, akamimina sadaka ya kinywaji juu yake, pia akamimina mafuta juu yake. 15 rYakobo akapaita mahali pale Mungu alipozungumza naye Betheli.
Betheli maana yake Nyumba ya Mungu.


Vifo Vya Raheli Na Isaki

16 tKisha wakaondoka Betheli. Walipokuwa umbali fulani kabla ya kufika Efrathi, Raheli akaanza kusikia uchungu na alipata shida kuu. 17 uAlipokuwa katika shida hii katika kujifungua, mkunga akamwambia, “Usiogope, kwa sababu umempata mwana mwingine.” 18 vHapo alipopumua pumzi yake ya mwisho, kwa maana alikuwa akifa, akamwita mwanawe Benoni.
Benoni maana yake Mwana wa huzuni yangu.
Lakini babaye akamwita Benyamini.
Benyamini maana yake Mwana wa mkono wangu wa kuume.


19 yKwa hiyo Raheli akafa, akazikwa kando ya njia iendayo Efrathi (ndio Bethlehemu). 20 zJuu ya kaburi lake, Yakobo akasimamisha nguzo, ambayo mpaka leo inatambulisha kaburi la Raheli.

21Israeli akaendelea tena na safari yake na kupiga hema mbele mnara wa Ederi. 22Wakati Israeli alipokuwa akiishi katika nchi ile, Reubeni mwanawe alikutana kimwili na suria wa baba yake aitwaye Bilha, naye Israeli akasikia jambo hili.

Yakobo alikuwa na wana kumi na wawili:

23Wana wa Lea walikuwa:
Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Yakobo,
Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari na Zabuloni.
24 aaWana wa Raheli walikuwa:
Yosefu na Benyamini.
25 abWana waliozaliwa na Bilha mtumishi wa kike wa Raheli walikuwa:
Dani na Naftali.
26 acWana waliozaliwa na Zilpa mtumishi wa kike wa Lea walikuwa:
Gadi na Asheri.
Hawa walikuwa wana wa Yakobo, waliozaliwa kwake akiwa Padan-Aramu.

27 adYakobo akarudi nyumbani kwa baba yake Isaki huko Mamre, karibu na Kiriath-Arba (yaani Hebroni), ambapo walikuwa wameishi Abrahamu na Isaki. 28 aeIsaki aliishi miaka 180. 29 afKisha Isaki akapumua pumzi yake ya mwisho akafa, akakusanywa pamoja na watu wake akiwa mzee wa miaka mingi. Nao wanawe Esau na Yakobo wakamzika.

Copyright information for SwhNEN